Featured
Loading...

VIDEO::Majibu Ya Lowassa Alipoulizwa "Mliteta nini na rais?"+ Kauli 10 nzito alizotoa Mbowe.

 Ndugu wanahabari,

Tarehe 27 Julai ya mwaka huu Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ilitangaza azimio la kuanzisha harakati tulizozipa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA). Pamoja na mengine, azimio hili lilipitishwa kufuatia tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kupiga marufuku mikutano yote ya vyama vya siasa katika nchi yetu hadi mwaka 2020. Kama mnavyokumbuka, Kamati Kuu yetu iliteua siku ya Septemba Mosi, yaani kesho, kuwa ni siku rasmi ya kuanza kwa harakati za UKUTA ambazo zingejumuisha mikutano ya hadhara na maandamano ya amani nchi nzima.

Kufuatia azimio la Kamati Kuu ya CHADEMA, mambo mengi sana yametokea. Mengi ya mambo haya ni ya ajabu na ya kusikitisha sana. Tumemwona Rais wa Jamhuri ya Muungano, aliyekula kiapo cha ‘kuilinda, kuihifadhi na kuitetea’ Katiba yetu na Sheria zake, ‘akiikanyaga’ Katiba hiyo hadharani kwa kutishia kwamba mtu yeyote atakayefanya mikutano na maandamano ya amani ‘atakiona cha mtema kuni.’

Tumeshuhudia Jeshi la Polisi, ambalo lina wajibu kisheria wa kutoa ‘ulinzi na msaada’ ili kuwezesha mikutano kufanyika kwa amani na utulivu, likizunguka mitaani mijini na vijijini na kutembeza hadharani magari ya deraya na silaha nyingine nzito za kivita kwa lengo la kuwatisha wananchi wanaopanga kutekeleza kile ambacho Katiba na Sheria za Tanzania zinawaruhusu kukifanya, yaani, mikutano ya hadhara na maandamano ya amani.

Tumeona kwa mshangao mkubwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likitoa tamko la vikosi vyake vyote nchi nzima kufanya usafi siku ya Septemba Mosi, wakati Jeshi hilo lilikwishafanya maadhimisho rasmi ya Sikukuu ya Mashujaa tarehe 25 Julai. Na tangu alfajiri ya leo hadi muda huu, JWTZ imerusha ndege za kivita katika maeneo yote ya Dar es Salaam, kitu ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya majeshi yetu.

Na wote tu-mashahidi wa jinsi ambavyo viongozi wa ngazi zote wa CHADEMA na wanachama wa kawaida wamekamatwa, kuteswa na kufunguliwa mashtaka ya uonevu kwa sababu tu ya kutetea au kutekeleza haki na uhuru wao kwa mujibu wa Katiba yetu. Aidha, tumeona matukio mabaya ya kihalifu – ya kweli ama ya kutengenezwa – yakihusishwa kwa makusudi na UKUTA ili kutengeneza mazingira ya kiusalama ya kuhalalisha ukiukwaji wa Katiba na Sheria zetu na vitendo vya kutesa waTanzania na kukiuka haki zao za binadamu.

Vile vile, kila mmoja wetu ameona sio tu mikutano ya hadhara na maandamano ya amani, ambayo imewekewa utaratibu wa kisheria, bali pia mikutano ya ndani ya vyama vya siasa, ambayo haijawekewa utaratibu wowote wa kisheria, ikikatazwa na Jeshi la Polisi. Mahali pengi katika nchi yetu, mikutano ya CHADEMA ya aina hiyo imevamiwa na kuvunjwa na Jeshi la Polisi na viongozi na wanachama wetu kukamatwa ama kupigwa na kuumizwa vibaya.

Ni juzi tu kikao cha pamoja cha Kamati Kuu yetu na Wabunge wetu kimevamiwa na polisi na viongozi wa ngazi za juu wa Chama kama vile Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mh. Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dkt. Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu John Mnyika na wajumbe wa Kamati Kuu Mh. Edward Lowassa na Prof. Mwesiga Baregu kukamatwa na kuhojiwa na polisi.

Na hivyo tunavyozungumza, Naibu Katibu Mkuu wetu Zanzibar, Mheshimiwa Salum Mwalimu na viongozi wengine wa chama chetu, wako rumande Bariadi mkoani Simiyu tangu wiki iliyopita, kwa sababu ya kunyimwa dhamana kwa kosa ambalo sheria iko wazi kwamba lina dhamana.

Sio tu uhai wa mfumo wa vyama vingi vya siasa ambao uko hatarini. Uhuru wa vyombo vya habari umeshambuliwa sana katika kipindi hiki. Ndani ya mwezi huu mmoja, gazeti la Mseto limefungiwa na vituo vya radio vya Radio 5 ya Arusha na Magic FM ya Dar es Salaam vimefungiwa kwa kutangaza habari zinazohusu UKUTA.

Ndugu wanahabari,
Yaliyofanywa na Rais Magufuli mwenyewe na Jeshi la Polisi yamefanywa pia na viongozi wa serikali wa ngazi za chini ya Rais, kama vile mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya. Hawa nao wametoa matamko ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara na kutoa amri za kuwakamata viongozi na wanachama wetu watakaofanya mikutano hiyo. Taasisi za nchi yetu ambazo zina wajibu wa kulinda haki za vyama vya siasa na haki za binadamu kwa ujumla zimejionyesha wazi wazi kutokuwa na uhuru unaohitajika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kisheria na kikatiba.

Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, ana wajibu wa kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo, ameshindwa kabisa kulinda na kutetea haki za vyama vya siasa za kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ya amani. Badala yake, Msajili Francis Mutungi amejidhihirisha kuwa adui mkubwa wa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi katika nchi yetu, kwa kuunga mkono matamko batili ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano ya amani.

Kwa kifupi, katika kipindi cha takriban mwezi mmoja tangu kutangazwa kwa UKUTA, tumeshuhudia Tanzania yetu ikiserereka kwa kasi kwenye mteremko mkali wa utawala wa kidikteta.

Ndugu wanahabari,
Katika mazingira haya, taifa letu limeingia katika taharuki kubwa. Watanzania wa kila rika na wa kila kundi la kijamii wameingiwa na hofu kubwa ya nchi yetu kuingia katika machafuko ya kisiasa na umwagaji damu mkubwa endapo siku ya Septemba Mosi, yaani kesho, tutatekeleza azimio letu la kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ya amani nchi nzima, na majeshi ya ulinzi na usalama yakatekeleza azma yao ya kutumia mabavu ya kijeshi kuzuia au kuzima mikutano na maandamano hayo ya amani.

Ndugu wanahabari,
Kwa sababu ya taharuki hii na ombwe kubwa la uongozi wa kisiasa lililojitokeza tangu tutangaze UKUTA, viongozi wakuu wa kidini wa madhehebu mbali mbali ya dini zote kubwa hapa nchini, yaani, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Tanzania, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Katibu Mkuu wa Baraza la Kikristo Tanzania (CCT), Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT), Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste ya Karismatiki, Mufti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Mufti Mkuu wa Zanzibar, wametuomba na kutusihi, katika vikao mbali mbali tulivyofanya pamoja nao, tuwape muda wa wiki mbili au tatu, ili waweze kufanya jitihada za kuonana na Rais Magufuli kwa lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huu wa kisiasa, ili kuliepusha taifa letu na machafuko ya kisiasa na umwagaji damu, utakaosababishwa na matumizi ya nguvu za kijeshi yanayotishiwa na Rais Magufuli na majeshi yetu ya ulinzi na usalama.

Aidha, sio viongozi wa kidini tu ambao wametuomba kuahirisha UKUTA kwa muda. Viongozi wa taasisi za kiraia kama vile Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Jukwaa la Wahariri na Jukwaa la Katiba nao wametusihi tuahirishe UKUTA kwa muda, ili tutoe fursa kwa jitihada za mazungumzo na majadiliano kufanyika.

Sisi CHADEMA tunatambua na kujali haki zetu za kisiasa kama zilivyofafanuliwa katika Katiba na Sheria za nchi yetu. Hata hivyo, tunajali na kuheshimu kwa kiasi kikubwa zaidi, haki ya waTanzania ya ‘kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yao’ kama ilivyotamkwa na ibara ya 14 ya Katiba. Tunatambua mchango mkubwa ambao umetolewa na dini zote hapa nchini katika kutunza utulivu uliopo Tanzania na katika ustawi wa kiuchumi na kijamii wa waTanzania. Tunaelewa rai ya viongozi wetu wa kiroho juu ya umuhimu wa kutafuta suluhu ya mgogoro huu wa kisiasa kwa mazungumzo na majadiliano.

Tofauti na wengine ambao wamekataa hata kuwaona viongozi wetu wakuu wa kidini, sisi tunawaheshimu viongozi wetu wa kidini. Tumekutana nao. Tumesikiliza na kutafakari wito wao wa kuahirisha UKUTA kwa wiki mbili au tatu, ili wapate fursa ya kuzungumza na Rais Magufuli na Serikali yake. Huu ni wito wa busara na wenye kulijali taifa letu na watu wake. Sio wito unaopaswa kupingwa kwa sababu nyepesi nyepesi.

Tofauti na wengine, sisi wa CHADEMA hatuwezi kuwakaidi viongozi wetu wa kidini katika wito wao huu wa busara.

Kwa sababu hizi zote, tunaomba kuwatangazia viongozi wetu wa ngazi zote za CHADEMA, pamoja na wanachama, wafuasi na mashabiki wetu na waTanzania wote popote walipo, kwamba tunaahirisha kwa mwezi mmoja mikutano na maandamano ya amani yaliyopangwa kufanyika nchi nzima kuanzia kesho Septemba Mosi, ili kutoa nafasi kwa viongozi wetu wa kiroho kutafuta suluhu ya jambo hili kwa kukutana na Rais Magufuli na Serikali yake.

Endapo jitihada za viongozi wetu wa kidini hazitazaa matunda katika kipindi hicho, mikutano na maandamano hayo ya amani sasa yatafanyika kuanzia Oktoba Mosi ya mwaka huu. Tunawaomba viongozi na wanachama wetu nchi nzima waendelee na maandalizi mbali mbali kwa ajili ya UKUTA katika maeneo yao.

Aidha, tunarudia wito wetu kwa vyama vingine vya siasa, taasisi na mashirika ya kiraia yasiyokuwa ya kiserikali, taasisi za kitaaluma za aina mbali mbali, vyombo vya habari na waTanzania katika ujumla wao, kujiunga na UKUTA na kutetea Katiba yetu na haki za binadamu. Tunasisitiza tena: hakuna atakayepona endapo Rais Magufuli atafanikiwa kuangamiza mfumo wa vyama vingi vya siasa katika nchi yetu kama alivyodhamiria.

Hakuna atakayekuwa salama endapo Rais Magufuli ataruhusiwa kukanyaga Katiba yetu, kupuuza sheria za nchi yetu na kukiuka haki zetu za binadamu kama anavyotaka. Kama inavyotamka Katiba yetu, ‘kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi.’ UKUTA ni sehemu ya hatua hizo za kisheria za kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria zetu. Tujenge UKUTA ili tuokoe nchi yetu.

--------------------------------

FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB)
MWENYEKITI TAIFA

 ZAIDI SIKILIZA VIDEO HIZI MBILI TOFAUTI
 
VIDEO. 1 


VIDEO. 2

Mwenyekiti wa CHADEMA taifa ameongelea uamuzi wa jeshi la wananchi kufanya usafi na urushaji wa ndege siku ya leo ambayo anasema haijawahi kufanya tangu uhuru.
Amesema anavyozungumza, katibu mkuu(Salum Mwalimu) anaendelea kushikiliwa na polisi mji wa Bariadi na ilikuwa leo apelekwe mahakamani lakini polisi wamesema wako bize.

Freeman Mbowe amesema maandamano ya UKUTA yameahirishwa kwa mwezi mmoja hadi tarehe Oktoba Mosi.

Mbowe: Tumepata wakati mgumu kufikia uamuzi, sio kila wakati viongozi tutafanya mambo yatayowapendeza wanachama wetu. Viongozi wa dini awali walikuja na ajenda moja, kuomba wabunge wa UKAWA warejee bungeni. Kamati kuu ya CHADEMA imepokea kwa heshima sana wito wa viongozi wa dini.

Mbowe: Ni matumaini yangu wana CHADEMA watatuelewa kamati kuu, asanteni sana kwa kunisikiliza.

Kinachoendelea kwa sasa ni maswali kutoka kwa waandishi wa habari.


Swali la mwandishi wa habari kwa Mbowe-Kwa nini hamjapeleka shauri mahakamani: 
Mbowe: Yamepelekwa mashauri mengi mahakamani na yataendelea kupelekwa. Hatuwezi kuwalazimisha mahakama, hata kipindi hiki kuna mashinikizo kwa baadhi ya mahakama watoe maamuzi watoe maamuzi yanayorandana na serikali, wapo waliosimamia sheria lakini mahakimu nao ni binadamu.
Mimi ni miongoni mwa watu ambao tulitamani kesho watu wawe barabarani, wanachama wetu ambao watakwazika, UKUTA sio CHADEMA, UKUTA ni mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya watanzania. Sasa hayo makundi yamekuja kutushauri tuwe pamoja, sisi ni nani tukatae. Watu kama Mwl Nyerere foundation wametusihi, hata Lowassa ameongea na mama Maria Nyerere wametusihi.

Mbowe: Viongozi waliomba wiki mbili mpaka tatu lakini sisi tukasema hapana kuna wengine tutakuwa na majukumu bungeni na hili jambo ni la kitaifa. Hatuna nia ya kuchafua Taifa, tuna nia ya kusaidia Taifa.

Mbowe: Mpaka jana tulikuwa na viongozi 230 amabao wameshtakiwa, viongozi 28 mapaka jana walikuwa hawajaachiwa kwa mujibu wa takwimu zetu akiwemo naibu katibu mkuu Zanzibar.

Mbowe: Nisikitike siku za karibu mahasimu wetu wamekuwa wakijaribu kutugombanisha ndani ya CHADEMA, hizi fitna za mitandao. Mbowe sina tabia ya kutoa matakamko nje ya taratibu za chama, Tamko nililotoa ni la leo.

Lowassa: Mitandao inaandika mambo mengi sana ambayo ni just accusations, ningekua na muda ningefafanua.

Lowassa Afunguka Mazito Kuelekea Kesho(Sept 1)

Nimelazimika kushika kalamu na kuandika masikitiko yangu,kwa jinsi serikali ya CCM inavyoelekea kulitumbukiza taifa letu katika mkwamo na machafuko ya kisiasa.
Sote tunafahamu hali ya kisiasa ilivyo tete kwa sasa hapa nchini.Serikali inaukandimiza upinzani na demokrasia kwa jumla.Tumelazimika kutangaza operesheni UKUTA kupinga ukandamizaji huo.
Binafsi nafurahishwa na kutiwa moyo na jinsi watanzania walivyoipokea operesheni hii,pamoja na vitisho vya dola.Siku zote sisi CHADEMA na UKAWA Kwa ujumla ni wenye kulitakia amani na utulivu taifa letu.Maandamano haya ya Sept mosi ni ya amani, lakini vitendo vya jeshi la Polisi vimewapa wasiwasi watanzania.
Nimepokea Simu nyingi sana kutoka kwa viongozi wastaafu na watu wengine mashuhuri na wa heshima kubwa hapa nchini kututaka tuzungumze na serikali ili kuliepusha taifa letu kutumbukia katika machafuko.
Tumeanza juhudi hizo, nyote ni mashahidi wa tukio la kukutana na Rais Magufuli katika jubilee ya miaka 50 ya ndoa ya Mzee Mkapa.Ulikuwa ni mwanzo wa juhudi zetu za kuwanyooshea wenzetu mkono wa amani.
Lakini cha kushangaza wenzetu hawako tayari kuupokea mkono huo.Jana(jumatatu) tukiwa katika kikao cha kujadiliana jinsi ya kuunyosha zaidi mkono huo, jeshi la Polisi likaja na kuukata mkono huo kwa kutukamata.
Kitendo kile kwangu binafsi kimezidi kuniimarisha na kunipa nguvu zaidi ya kudai demokrasia na kuheshimu katiba ambayo viongozi wetu waliapa kuifuata na kuitetea.

Edward Ngoyai Lowassa
Mjumbe wa kamati Kuu CHADEMA

KUONA VIDEO YAKE BONYEZA HAPA CHINI KWENYE PICHA KUSIKIA NA AMBAYO HAYAJAANDIKWA

Katuni 5 Zilizotikisa Leo-SIASA & MICHEZO & MAISHA
Premier League Standings(Msimamo EPL)

Taarifa ya uteuzi wa Bodi ya Wakurugenzi NDC

TANESCO: Maeneo yatakayokosa umeme kati ya Septemba 3 na 25

Magazetini Leo Jumatano 31, August 2016

IMG_20160831_051851
IMG_20160831_051904
IMG_20160831_051919
IMG_20160831_051931
IMG_20160831_051943
IMG_20160831_051956
IMG_20160831_052009
IMG_20160831_052021
IMG_20160831_052032
IMG_20160831_052044
IMG_20160831_052055
IMG_20160831_052106
IMG_20160831_052117
IMG_20160831_052127
IMG_20160831_052139
IMG_20160831_052150
IMG_20160831_052201
IMG_20160831_052212
IMG_20160831_052223
IMG_20160831_052233
IMG_20160831_052247
IMG_20160831_052258
IMG_20160831_052320

KONDOM MILIONI 21 KUGAWANYWA TANZANIA


 
 

Serikali ya Tanzania imeanza zoezi la kugawanya kondomu milioni 21 kwa watanzania ili kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya HIV.

Kondomu hizo zitaganywa bureee.

Wizara ya afya na maendeleo ya jamii Tanzania imesema mpango huo maalum ni lengo la pamoja la mataifa mbali mbali kufanya bidii kumalizana na ukimwi kufikia 2030.

Nape Ashushiwa Zigo Kuhusu Maamuzi Yake Haya IMG-20160830-WA0044.jpg


Katuni 5 Bora Za Leo-SIASA, MAISHA & MICHEZO


Baiskeli Kubwa Kuliko Zote Duniani(Picha 5)

German man builds a bicycle that weighs nearly a tonne at an attempt of entering the Guinness Book of World Records as the heaviest in the world.
Frank Dose spent 4,577 dollars on the bicycle weighing 940 Kgs beating the current heaviest that weighs 860kg. He is however putting more things on it to get to a tonne.
Dose has been putting the bicycle through testing to ensure it can travel 500 yards to clinch the world record reports the Daily Mail.
Picture courtesy Daily Mail

Older Posts
© Copyright FURAHIA MAISHA blog | Designed By 0755801248
Back To Top