Leicester City yamnasa Wilfred Ndidi kwa pauni milioni 15 | furahia.newz
Breaking News
Loading...

Leicester City yamnasa Wilfred Ndidi kwa pauni milioni 15

Klabu ya Leicester City wanatarajiwa kumnasa kiungo wa kati wa klabu ya Genk ya Ublegiji Wilfred Ndidi kwa pauni milioni 15, timu ambayo anaichezea mtanzania Mbwana Samata.
Klabu hizo tayari zimeafikiana kuhusu kuhama kwa mchezaji huyo na kilichosalia pekee ni kibali chake cha kufanyia kazi Uingereza. Mchezaji huyo mwenye miaka 20 kutoka Nigeria atatia saini mkataba wa miaka mitano na nusu atakapokamilisha uhamisho wake. Leicester, kwenye tovuti yao, wamethibitisha kwamba klabu hizo zimeafikiana na kwamba Ndidi amefanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Ndidi aliisaidia timu yake Genk kumaliza wa kwanza kundi lao la Europa League msimu huu na kufuzu kwa hatua ya muondoano.
 Image may contain: 1 person, playing a sport and outdoor

About Author
  • mwana habari Read More